Friday, September 14, 2012

Fid Q afikiria kuwapeleka kortini Orijino Komedi
Baada ya Orijino Komedi kumshutumu rapper Fareed Kubanda aka Fid Q kuwa amecopy na kupaste beat ya wimbo wake Danger, rapper huyo hajaridhika na hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kiasi cha kufikiria kutafuta mwanasheria ili awaburuze kortini waigizaji hao.
“Looking for a good lawyer dealing with defamation of character cases.. Contact us for details,” Fid alitweet jana.
Baada ya kuona tweet hiyo, Bongo5 ilimpigia simu rapper huyo kutaka kujua kama kweli amedhamiria kulipeleka suala hilo kwenye sheria na yeye kusema kuna watu walimshauri afanye hivyo lakini ameamua kupuuzia.
Hata hivyo alisema suala hilo limemuumiza kwakuwa watu wasiofahamu masuala hayo wamemchukulia tofauti.
“And you know one of the things that I hate nowdays is taking everything for granted. Unajua kilichoniuma ni kwamba ingekuwa Ulaya, watu Ulaya wanajua lakini sasa Bongo unapowaambia hivyo watu wanaamini hundred percent,” alisema.
Aliongeza kuwa amekuwa akipata ujumbe kupitia Facebook unaomkera kwakuwa watu wamepotoshwa na Orijino Komedi.
Staa huyo wa ‘Sihitaji Marafiki, aliiambia Bongo5 kuwa atahitaji Orijino Komedi wamemuombe radhi rasmi kwa kuchafua jina lake.
Wiki hii studio iliyotengeneza beat hiyo iliamua kutoa tamko na kuwashutumu Orijino Komedi kwa kukurupuka kuongea kitu wasichokifahamu.
“Chofaco Records owns full copyright of the song Danger by Fid Q, produced by chobaray.Nyimbo ilirekodiwa November,2008,jiulizee nyimbo ilitoka mwaka gani?mziki wa USA sio sawa na mziki wa Bongo. Kuna tofauti kati ya mixtape songs and album songs also released tracks,non exclusive tracks and exclusive tracks,kabla orijino komedi kukurupuka na kuongea/kufanya vipindi vyao lazima mjue copyrights za kazi za watu,heshima na busara,kuuliza na kuelimishwa si ujinga.”

JUMA NATURE ADAIWA KUMTELEKEZA MTOTO WAKE.Juma Nature.
Samson mtoto anayedai Juma Nature ni baba yake.
Juma Kassim Ally alias Juma Nature ambaye ni Hip Hop Artist na Singer toka Tanzania pia ni founder na member wa kundi la Wanaume Halisi hivi karibuni amekutwa na tuhuma za kumtelekeza mwanae wa kiume.
Kutokana na swala hili, hitmaker wa “Hili Game” anaweza akajikuta matatani soon na Ustawi wa jamii baada ya kumkataa mtoto anayedai msanii huyo ni baba yake mzazi.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 17 aitwaye Samson Juma Kassim Kiroboto ameamua kusafiri toka mkoani Morogoro na kuja Dar es Salaam kuweza kumfata Baba yake.
Samson alilazimika kwenda Clouds Fm Radio ili aweze kupata msaada kwa jinsi atakavyoweza kumpata baba yake huyo, anasema mama yake alishafariki Dunia hivyo anamuhitaji Baba yake ili maisha yaendelee.
Hata hivyo katika jitihada za Kumtafuta Juma Nature, Samson anasema “mama yangu ameshafariki na nilishawahi kwenda mpaka kwa baba yangu Juma Temeke nikiwa na bibi yangu, lakini aliponiona tu akanifukuza akasema hataki kuniona tena “.

JACK PATRICK AACHIA PICHA NYINGINE ZA NGONO

MLIMBWENDE mtata Bongo, Jacqueline Patrick, kama kawa, amedondosha picha nyingine chafu kwenye ‘peji’ yake ya mtandao wa BBM.

Jack ambaye ni mke wa mfanyabiashara Abdulatif Fundikira alitupia picha hizo Julai 25, mwaka huu huku akizisindikizia na ujumbe usemao ‘sina tatizo na mtu na mwenye macho haambiwi tazama.’

Picha hizo zimezua maswali mengi kwa watu wake wa karibu ambao wengi ni waumini wa dini ya kisilam ambao kwa mwezi huu wapo ndani ya swaumu.
Wengi walihoji nini kilimfanya staa huyo kuweka picha hizo chafu sana zenye kumwonesha kila kitu huku akiwa ameolewa kwa ndoa! “Au yuko sokoni zaidi?” alihoji mdau wake mmoja.

Jack bila kujali hilo aliendelea kuanika picha hizo kwa kubadilisha moja baada ya nyingine kulingana na mapozi aliyotaka mwenyewe

FAHAMU MAMBO 10 KUHUSU AGNESS MASOGANGE1: Umewahi kukaa kwa muda gani bila kuoga ?
Hahahahha duu! hii kali, nakumbuka when I was 15 niliwahi kukaa siku mbili maji hayayajui mwili wangu, usiniambie wewe hujawahi kufanya hivi.
2: Between Obama and Kikwete is hotter?
Wewe My president is hottest prezzo in the world. JK is the one.
3: The best part of your body is………….
My figure, namshukuru sana mungu kwa kuniumba hivi.
4: Kitu gani ambacho unahisi cha kijinga ulishawahi kufanya kwa sababu ya mapenzi?
Nakukumbuka kuna siku nililia mbele ya umati wa watu in the club baada ya mpenzi wangu kunizingua.
5: One night with Bongo celebrity – who’s the lucky guy?
My man DJ Choka coz Hugo ni mtu ambaye kila nikikutana nae huwa hanikwazi, muda ananifurahisha tu.
6: Ni umbea gani umeshawahi kuusikia kuhusu na ukakuudhi sana?
Kuna gazeti moja la udaku liliwahi kuandika kwamba ninatumia dawa za kichina kutengeneza shepu yangu, hilo suala liliniudhi coz halikuwa na ukweli wowote na watu wanaonifahamu tangu nikiwa mdogo ni mashahidi.
7: The last man you met last night, who’s he?
Ofcourse ni my baby – ndio mwanaume mwisho kuiona sura yangu jana usiku.
8: Celebrity wa kike wa Bongo ambaye anayekufanya utamani kuwa mwanaume?
Hahahahaha hii noma! I think Wema Sepetu is very beautiful, she can drive crazy any man.
9: What turns you on in a man?
Jamani mie mdhaifu kwa mwanaume anayenukia vizuri.
10: Kati ya Diamond Platnumz na Gelly wa Rhymes nani unafikiri anajua sana mapenzi?
Duu nyiee! anyway kwa upande wangu I think Gelly knows how to handle a woman

MIMBA YA JINI KABULA YACHOOPOKA
SIKU chache baada ya kuahidi kumzalia mtoto mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Bushoke, mwigizaji wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amedaiwa kupata tatizo la mimba yake kuharibika.

Chanzo chetu kimetutonya kuwa, kuharibika kwa mimba hiyo kulibainika hivi karibuni huku mwenyewe akieleza kutojua sababu.

“Mwenyewe anadai hata hajui imeharibika kwa sababu gani lakini ukweli ndiyo huo.Hata alipohojiwa na Clouds Tv juzi alishindwa kunena ukweli.Kwa sasa hana raha kabisa kwani alishaamua kuzaa lakini ndiyo hivyo tena,” kimedai chanzo hicho.

Katika kupata ukweli wa habari hiyo, mwandishi wetu amemtafuta Jini Kabula na alipoulizwa juu ya mimba yake kuchoropoka amesema kwa masikitiko:

“Naomba unipigie baadaye nitakueleza kila kitu lakini ni ukweli kwamba ‘mwanangu’ ametoka.”

WAKUVANGA AGEUKIA MUSIKI

Baada ya kuonyesha uwezo kwenye tasnia komedi nchini, Msanii maarufu wa vichekesho kutoka kundi la Orijino Komedi kwa jina la Wakuvanga ameamua kubadili fani na kuamua kujitosa kwenye fani ya muziki. Msanii huyo amekamilisha albam yenye nyimbo tisa na kutengeneza video zake katika albamu alioipa jina la “Kato“.

Alitaja baadhi ya nyimbo katika albamu hiyo kuwa ni Angwisa, Ndoa, Anacheza, Analia na Viatu sio watu. Akiongea mwishoni mwa wiki Wakuvanga aliwataka mashabiki wake waipokee albamu hiyo pindi itapokuwa sokoni.

Kutokana na Wakuvanga kuingia kwenye fani ya Muziki amefanya idadi ya wasaniii wa kundi ilo kuongezeka baada ya wasanii wenzake watatu wa kundi hilo Joti, Mpoki kufanya muziki kwa sasa, bila kumsahau Masanja ambaye anaimba nyimbo za Injili.

NIKKI MBISHI AKANA KUMDISS LOVENESS LOVE
Rapper anayeheshimika kwa uandishi mkali wa mashairi na mchawi wa freestyle Tanzania, Nikki Mbishi, amekanusha kumdiss mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Loveness Diva, katika wimbo wake uitwao ‘Feedback’ uliopo kwenye albam yake, Jogoo.

Mstari huo unasema, “Hauwezi kuiva mpaka uwe unamskiliza Loveness Love,Kicheche unajiita diva hiyo ni nonsense kavu.”


Hata hivyo akiongea na 255 ya Clouds FM jana, rapper huyo amesema mlengwa wa mstari huo sio mtangazaji huyo bali ni ex wake aliyemzingua.

“Huo mstari nilimchanaga mtu mmoja ambaye niliwahi kuwa na uhusiano naye akanizingua, halafu sehemu aliyokuwa anatumia kijifunza mapenzi ni kile kipindi cha Loveness Love, ndo maana nikamuuliza huwezi kuiva kimapenzi mpaka uwe unamsikiliza Diva?

Umeona, kwahiyo yeye sasa mwisho wa siku ikafika hatua hadi anajiita diva, nikamwambia wewe ni kicheche unajiita diva?

Halafu hiyo ni nonsense kavu yaani, sababu haina maana wala misingi yoyote katika uhusiano wangu mimi na wewe, ndo maana ya huo mstari, lakini haikuwa direct kwamba namchana Love sijui ni nini,hapana yeye hahusiki na wala hajui nini maana ya huo mstari yaani," alisema Nikki Mbishi.