Friday, September 14, 2012

JUMA NATURE ADAIWA KUMTELEKEZA MTOTO WAKE.



Juma Nature.
Samson mtoto anayedai Juma Nature ni baba yake.
Juma Kassim Ally alias Juma Nature ambaye ni Hip Hop Artist na Singer toka Tanzania pia ni founder na member wa kundi la Wanaume Halisi hivi karibuni amekutwa na tuhuma za kumtelekeza mwanae wa kiume.
Kutokana na swala hili, hitmaker wa “Hili Game” anaweza akajikuta matatani soon na Ustawi wa jamii baada ya kumkataa mtoto anayedai msanii huyo ni baba yake mzazi.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 17 aitwaye Samson Juma Kassim Kiroboto ameamua kusafiri toka mkoani Morogoro na kuja Dar es Salaam kuweza kumfata Baba yake.
Samson alilazimika kwenda Clouds Fm Radio ili aweze kupata msaada kwa jinsi atakavyoweza kumpata baba yake huyo, anasema mama yake alishafariki Dunia hivyo anamuhitaji Baba yake ili maisha yaendelee.
Hata hivyo katika jitihada za Kumtafuta Juma Nature, Samson anasema “mama yangu ameshafariki na nilishawahi kwenda mpaka kwa baba yangu Juma Temeke nikiwa na bibi yangu, lakini aliponiona tu akanifukuza akasema hataki kuniona tena “.

0 comments:

Post a Comment