Friday, September 14, 2012

MIMBA YA JINI KABULA YACHOOPOKA




SIKU chache baada ya kuahidi kumzalia mtoto mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Bushoke, mwigizaji wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amedaiwa kupata tatizo la mimba yake kuharibika.

Chanzo chetu kimetutonya kuwa, kuharibika kwa mimba hiyo kulibainika hivi karibuni huku mwenyewe akieleza kutojua sababu.

“Mwenyewe anadai hata hajui imeharibika kwa sababu gani lakini ukweli ndiyo huo.Hata alipohojiwa na Clouds Tv juzi alishindwa kunena ukweli.Kwa sasa hana raha kabisa kwani alishaamua kuzaa lakini ndiyo hivyo tena,” kimedai chanzo hicho.

Katika kupata ukweli wa habari hiyo, mwandishi wetu amemtafuta Jini Kabula na alipoulizwa juu ya mimba yake kuchoropoka amesema kwa masikitiko:

“Naomba unipigie baadaye nitakueleza kila kitu lakini ni ukweli kwamba ‘mwanangu’ ametoka.”

0 comments:

Post a Comment